Nairobi. Marekani yaonya kuhusu ugaidi na uharamia.
24 Septemba 2005Matangazo
Marekani imerudia tena onyo lake dhidi ya ugaidi katika mataifa ya Afrika mashariki, ikiwatahadharisha raia wa Marekani dhidi ya uwezekano wa mashambulizi ya kigaidi pamoja uharamia wa baharini katika eneo la pwani ya nchi hizo ambako matukio ya utekaji nyara meli yameripotiwa.
Wiki tatu kabla ya kumalizika muda wa tahadhari yake ya mwanzo iliyotolewa hapo Julai mosi, wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani jana Ijumaa ilitoa tahadhari nyingine katika eneo hilo la Afrika mashariki, likilenga hasa katika ongezeko la uharamia baharini.