Mzozo wa kisiasa Kenya | NRS-Import | DW | 16.02.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

NRS-Import

Mzozo wa kisiasa Kenya

Hakuna mwafaka wa kugawana madaraka uliofikiwa Kenya

NAIROBI
Serikali ya Kenya na chama kikuu cha upinzani wamekubaliana kuunda tume huru ya kuchunguza mgogoro wa matokeo ya uchaguzi wa Desemba mwaka jana yaliyomrudisha madarakani rais Mwai Kibaki.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan alitoa tangazo hilo baada ya kuongoza mazungumzo ya siku mbili juu ya suala hilo kati ya serikali na chama cha bwana Raila Odinga cha ODM.Aidha Kofi Annan alikiri kwamba masuala yanayozungumziwa ni mengi na magumu lakini ana matuamini kwamba pande hizo mbili zinazozozana kuhusu madaraka zitaafikiana kuunda serikali ya mseto.Mazungumzo hayo ya suluhu yataanza tena jumanne ijayo.Matokeo ya uchaguzi wa rais hapo mwezi Desemba ambayo upinzani unasema yalikuwa ya uongo yalizusha mapigano makali ya kikabila na kusababisha kuuwawa kwa watu zaidi ya 1000 nchini Kenya na kuwaacha maelfu ya wengine bila makaazi.

 • Tarehe 16.02.2008
 • Mwandishi Ramadhani Yusuf, Saumu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8Nx
 • Tarehe 16.02.2008
 • Mwandishi Ramadhani Yusuf, Saumu
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/D8Nx
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com