MOSCOW : Urusi yatangaza maombolezo ya kitaifa | Habari za Ulimwengu | DW | 24.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW : Urusi yatangaza maombolezo ya kitaifa

Rais Vladimir Putin wa Urusi ametangaza siku ya maombolezo ya taifa hapo kesho wakati rais alliemtangulia Boris Yeltsin atakapozikwa kwa heshima zote za taifa.

Yeltsin amefariki kutokana na mshtuko wa moyo hapo jana akiwa na umri wa miaka 76.Hapo mwaka 1991 Yeltsin alikuwa rais wa kwanza aliechaguliwa kidemokrasia na alitumikia wadhifa huo hadi mwishoni mwa mwaka 1999.Amekuwa akipongezwa kwa kuiweka Urusi kwenye njia ya demokrasia na uchumi unaotegemea nguvu za soko.

Hata hivyo Warusi wengi watakuwa wanamkumbuka zaidi kwa kuzorota vibaya kwa uchumi wa nchi hiyo katika miaka ya 1990 wakati wa uongozi wake.Yeltsin pia ameiongoza Urusi katika vita vya kwanza dhidi wa waasi wanaotaka kujitenga huko Chechnya ambavyo vilimalizika kwa Urusi kuondowa wanajeshi wake kwenye jimbo hilo.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amempongeza Yeltsin kuwa mtetezi wa demokrasia na uhuru na kwamba alikuwa rafiki wa kweli kwa Ujerumani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com