Mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni na ulinzi waanza mjini Brussel. | Matukio ya Kisiasa | DW | 17.11.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni na ulinzi waanza mjini Brussel.

Mkutano maalum wa umoja wa Ulaya uliokuwa na lengo la kuwapata wagombea watakaochukua nyadhifa za juu za umoja wa Ulaya, baada ya kuhitilafiana umeahirishwa.

default

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg.

Mkutano maalum wa umoja wa Ulaya uliokuwa na lengo la kuwapata wagombea watakaochukua nyadhifa za juu za umoja huo, kutokana na kuhitilafiana kukubwa umeahirishwa. Amesema hayo Cecilia Malmström jana Jumatatu ,waziri wa Sweden katika umoja wa Ulaya , ambaye nchi yake inashikilia kwa hivi sasa urais wa umoja wa Ulaya, baada ya majadiliano ya mawaziri wa mambo ya kigeni mjini Brussels. Iwapo hakutakuwa na muafaka wakati wa kikao cha viongozi wa nchi na serikali siku ya Alhamis kuhusiana na wadhifa wa rais wa baraza la Ulaya na mwakilishi wa umoja wa Ulaya katika mambo ya nje, mkutano huo utaendelea kwa dharura.

Hali ya kutabiri inaendelea. Nani atakuwa rais wa baraza la Ulaya na nani atakuwa mwakilishi wa mambo ya kigeni wa umoja huo. Katika mkutano maalum siku ya Alhamis mjini Brussels viongozi wa nchi na serikali watalazimika kuamua kuhusu nyadhifa hizo za juu. Waziri mkuu wa Swden Fredrik Reinfeldt analishughulikia suala hili bila kuchoka kwa ajili ya mataifa yote. Lakini waandishi wa habari hawakuweza kupata siri mpya.

Hakuna majina - Najua kuwa mna shauku kubwa, lakini sina lolote nijualo kuhusu orodha ya majina na waziri mkuu hayuko tayari. Kwa hiyo anazungumza na wenzake.

Malmström amesema hapo kabla kuwa huenda nyadhifa zote zikachukuliwa na wanawake, lakini kwa bahati mbaya kuna wanawake wachache sana wanaowania nafasi hiyo.

Mawaziri wa ulinzi wamejikita katika suala Afghanistan , ambalo si tu katika kiwango cha kijeshi lakini pia hata kwa upande wa raia ni suala linalojadiliwa. Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Karl-Theodor zu Guttenberg hakuweka msimamo wake siri, kwamba serikali ya Afghanistan inalazimika kuchukua hatua nyingi zaidi.

Matarajio ni makubwa mno kwa utawala huu mpya, kwamba inapaswa kupambana na rushwa, na uhalifu na sio kwa maneno tu, na kwamba inapaswa pia kupambana na madawa ya kulevywa. Huu ni mtazamo mpana, na tunalazimika kutekeleza na sio kusema maneno tu.

Siku mbili kabla ya mkutano baina ya umoja wa Ulaya na Urusi pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kuwa na mfumo wa tahadhari na mapema. Umoja wa Ulaya , unashaka kuwa huenda katika majira yajayo ya baridi Urusi ikasitisha ugavi wake wa gesi. Sababu ya kusitishwa ugavi huo mwanzoni mwa mwaka huu ni mvutano wa malipo kati ya Urusi na Ukraine ambapo bomba linalopitisha gesi linapitia nchini humo.

Mwandishi Hasselbach, Christoph / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri Mohammed Abdul Rahman

 • Tarehe 17.11.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KYw4
 • Tarehe 17.11.2009
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KYw4
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com