Mkondo mpya katika mzozo wa Syria | Magazetini | DW | 10.09.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Mkondo mpya katika mzozo wa Syria

Mzozo wa Syria na uwezekano wa kusaka ufumbuzi wa kisiasa pamoja na kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani ndizo mada kuu magazetini .

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry

Mzozo wa Syria na uwezekano wa kusaka ufumbuzi wa kisiasa pamoja na kampeni za uchaguzi nchini Ujerumani ndizo mada kuu magazetini hii leo.

Tunaanza bila ya shaka na hali inayoashiria kubadilika katika mzozo wa Syria na hasa kuhusiana na uwezekano wa Marekani na washirika wake kuirudi Syria kwa dhana za kutumia gesi za sumu dhidi ya raia wasiokuwa na hatia.Gazeti la Hessische Niedersächsische Allgemeine linaandika:

Marekani bado haijatoa ushahidi bayana unaonyesha serikali ya Assad ina hatia.Bado pia haijulikani kwa uhakika nani amekiuka mstari mwekundu.Vipi mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel anaweza kuepuka kizungumkuti cha kumtia adabu mtu ambae pengine hana hatia,eti tu kwasababu wamemuonya mapema?Barack Obama anabidi avute wakati hadi mambo yatakabobainika,na kuungwa mkono na walio wengi pamoja na washirika kuwa imara.Yadhihirika kana kwamba waziri wa mambo ya nchi za nje ameshaamua kujipa muda huo.Ikiwa Moscow na Syria wanaunga mkono kwa dhati pendekezo la John Kerry,silaha za kemikali kuikabidhi jumuia ya kimataifa-basi hapo Obama atajitoa mashakani.Hakutakuwa tena na haja ya kutupa mabomu kuitia adabu Syria.Hilo lakini halitabadilisha chochote katika mkondo wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.

Sergei Lawrow und Walid Muallem Treffen in Moskau

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lawrow na waziri mwenzake wa Syria Walid Muallem baada ya mazungumzo yao mjini Moscow

Jee Irashambuliwa au la?

Suala kama Syria iadhibiwe kwa kutumia gesi za sumu halijapata jibu bado:Bunge la Marekani-Congress linatazamiwa kuamua kuhusu hatima ya hatua za kijeshi dhidi ya utawala wa Bashar al Assad.Gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linaandika:

Uongozi ndio unaohitajika hivi sasa:Lakini wa kushika usukani ni nani-baada ya kiongozi mwenye nguvu kupita wote katika ulimwengu wa magharibi kuwatupia mpira mamia ya wawakilishi na maseneta?Na baada ya kila wakati karata za kisiasa kuchanganywa upya?Rais wa 44 wa Marekani ameingia madarakani akiahidi kujitenganisha na "mwongo wa vita" wa mtangulizi wake George W. Bush.Katika utawala wake lakini kumeibuka hivi sasa kitisho cha kuzuka vita.Ndo kusema kitisho hicho ni mbinu tu ili kuzipa nafasi juhudi za kidiplomasia?Au hautapita muda ,mabomu yataanza kuporomoshwa?Hakuna ajuaye!

Tür zu Tür Wahlkampf mit Karamba Diaby

Katibu mkuu wa SPD Andrea Nahles pamoja na Karamba Diaby katika kampeni yaao huko Halle-Mashariki ya Ujerumani

SPD watafanya nini baada ya Septemba 22?

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Ujerumani,watu wanalalamika wanasema ni chapwa.Vipi wapiga kura na hasa wale ambao mpaka sasa bado hawajaamua nani wampe kura zao,wanaweza kushawishika?Gazeti la Mannheimer Morgen" linaandika:

Licha ya majaribio yote ya kujongeleana chama cha SPD hadi wakati huu hakitaki asilan kusikia wafuasi wa mrego wa shoto die Linke wakitajwa.Wana Social Democratic watapoteza imani ya wapiga kura watakapojaribu baada ya uchaguzi kufikiria uwezekano wa kuunda muungano wa pande tatu za mrengo wa shoto.Suala linalozuka hapo ni jee,SPD kwa kuzingatia mkakati wa kisiasa,itaridhika na kukalia viti vya upinzani au itajiachia kuwa mshirika mdogo katika serikali ya muungano wa vyama vikuu?Jibu la suala hili bado halijulikani.Kwasababu kiu cha kuweza siku moja kumteuwa kansela ni kikubwa kwa namna ambayo haitakua ajabu kama SPD itafikiria uwezekano wa kushirikiana na die Linke.

Mwandishi:Hamidou Oummilkhweir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman