1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkataba wa Lisbon wapitishwa na baraza la wawakilishi Ujerumani

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E4sS

BERLIN

Baraza la wawakilishi wa serikali za majimbo nchini Ujerumani limeidhinisha mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya ambao unalenga kuleta mageuzi katika masuala yanayohusu maamuzi kwenye Umoja wa Ulaya.Mkataba huo wa Lisbon umeidhinishwa kirahisi na wingi wa thuluthi mbili na kupingwa na mjumbe mmoja tu.Mwezi Uliopita bunge la Ujerumani liliidhinisha kwa wingi katiba hiyo ambayo kansela Angela Merkel anaiunga mkono akielezea kama ni msingi mpya kwa Umoja wa Ulaya.Hata hivyo mkataba huo sasa unasubiri kutiwa saini na rais Horst Kohler.