Mjadala wazuka baada ya Ujerumani kukubali kuchukua wafungwa wa Guantanamo | Matukio ya Kisiasa | DW | 08.07.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mjadala wazuka baada ya Ujerumani kukubali kuchukua wafungwa wa Guantanamo

Ujerumani inataka kuwachukua wafungwa wawili wa jela ya Guantanamo. Amesema hayo waziri wa mambo ya ndani Thomas de Meiziere jana mjini Berlin. Hatua hiyo imezua mjadala mkubwa mjini Berlin.

Wafungwa wa jela ya Guantanamo kutoka kabila la Waigua kutoka China ambao wameonekana kutokuwa na makosa, lakini wameshindwa kupata nchi ya kuwapeleka kuishi, na hawawezi kurejea nyumbani nchini China.

Wafungwa wa jela ya Guantanamo kutoka kabila la Waigua kutoka China ambao wameonekana kutokuwa na makosa, lakini wameshindwa kupata nchi ya kuwapeleka kuishi, na hawawezi kurejea nyumbani nchini China.

Ujerumani inataka kuwachukua wafungwa wawili wa jela ya Guantanamo. Amesema hayo waziri wa mambo ya ndani Thomas de Meiziere jana Jumatano mjini Berlin. Uamuzi huo umeleta mjadala mkubwa mjini Berlin.

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International na lile la Human Rights Watch yameukaribisha uamuzi huo wa waziri wa mambo ya ndani. Na pia upande wa upinzani unaunga mkono uamuzi huo wa waziri Thomas de Maiziere, wa kuwachukua wafungwa hao wawili kutoka jela ya Guantanamo nchini Ujerumani. Dieter Wiefelspütz ni mtaalamu wa mambo ya ndani kutoka chama kikuu cha upinzani cha SPD.

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya Ujerumani alichofanya ni sahihi na kinachongia akilini. Kwa kutumia sheria ameweza kufanya kile ambacho marafiki zake katika chama wamekuwa wakikizuwia, na hapa nampongeza.

Hata chama cha kijani, The Greens kimekuwa mstari wa mbele katika kupigania kuwachukua wafungwa wa Guantanamo. Hata hivyo kiongozi wa kundi la wabunge wa chama hicho katika bunge la Ujerumani Volker Beck hakumsifu waziri huyo wa mambo ya ndani.

Uamuzi huo unakuja wakati muda umepita sana na amechukua tahadhari sana. Ujerumani ingeweza hapa kujishughulisha zaidi.

Mtangulizi wa De Maizieres , Schäuble amekuwa akisitisha mara kwa mara upokeaji wa wafungwa hao kutoka Guantanamo. Majimbo kadha ya Ujerumani yamekuwa yakikataa kuwachukua wafungwa hao. Ukosoaji dhidi ya mipango hiyo ulitokea katika miezi ya hivi karibuni hususan kutoka chama cha CDU na CSU. Waziri wa mambo ya ndani wa Bayern Joachim Herrmann anatanabahisha kuwa uamuzi huo una hali ya kuuma meno.

Suala la Guantanamo linaweza kujadiliwa kisheria. Ndio sababu wafungwa hao, kuwa huko sio jambo la hatari. Mwenye jukumu na jela ya Guantanamo ni Marekani na sio sisi Ujerumani.

Wafungwa wote hao wawili watapelekwa katika majimbo ya Rheinland Pfalz na Hamburg. Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Rheinland Pfalz Karl-Peter Bruch , anadai kuwa jimbo lake lilikuwa makao ya jeshi la Marekani na linawajibu maalum kwa Marekani . Julia Klöckner ni kiongozi wa CDU na kiongozi wa upinzani katika jimbo hilo.

Mimi binafsi siungi mkono mtazamo wa Bwana Bruch, ambaye ametoa ombi hilo kwa waziri wa mambo ya ndani ya serikali ya shirikisho, kwamba atamchukua mfungwa mmoja wa jela ya Guatanamo. Lakini ndio sababu hivi sasa ni muhimu kuangalia kwa dhati matatizo ya wananchi wa jimbo hili na kuangalia usalama wao.

Waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya Ujerumani anahakika, kwamba wafungwa wote hao wawili hawataleta kitisho. Pamoja na hayo wote wawili wataendelea kufuatiliwa. Kwa vyovyote vile Ujerumani inataka kuchukua wafungwa wengine zaidi. Kwa hivi sasa katika jela hiyo ya Guantanamo kuna wafungwa wapatao 180.

Mwandishi : Bölinger, Mathias/ ZR / Sekione Kitojo.

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman

E N D E

 • Tarehe 08.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OEH4
 • Tarehe 08.07.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OEH4
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com