MIRAN SHAH : Akatwa kichwa kwa kuifanyia ujasusi Marekani | Habari za Ulimwengu | DW | 20.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MIRAN SHAH : Akatwa kichwa kwa kuifanyia ujasusi Marekani

Wanamgambo wanaotuhumiwa kuwa wafuasi wa kundi la Taliban wamemkata kichwa mtu mmoja wanaemtuhumu kuwa mpelelezi wa Marekani.

Mauaji hayo ya kikatili yametokea katika jimbo la Waziristan ya Kaskazini nchini Pakistan karibu na mpaka na Afghanistan. Waasi kaskazini na eneo la jirani la Waziristan ya Kusini wameuwa madarzeni ya watu wanaotuhumiwa kuunga mkono serikali ya Pakistan au kufanya ujasusi kwa ajili ya Marekani.

Wakati huo huo wanajeshi wa Afghanistan na wale wa kimataifa wameuteka tena mji wa Bakwa ulioko kusini magharibi mwa Afghanistan ambao kwa muda mfupi ulikuwa kwenye mikono ya wanamgambo wa Taliban.

Waasi wa Taliban bado wanaushikilia mji wa kusini wa Musa Qala ambao waliuteka hapo tarehe pili mwezi wa Februari.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com