Miaka 20 ya kuporomoka ukuta wa Berlin | Muungano wa Ujerumani | DW | 19.10.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Muungano wa Ujerumani

Miaka 20 ya kuporomoka ukuta wa Berlin

Usovieti iliduwaa ilipoarifiwa kwamba ukuta wa Berlin umeporomoka

Trotz dieses Appells, gelingt es Hunderten von Oppositionellen am 7. Oktober im Zentrum der DDR-Hauptstadt an einer spontanen Kundgebung teilzunehmen. Dabei skandierten sie immer wieder den Namen von Gorbatschow. Dutzende von Demonstranten werden von der Volkspolizei und von Stasimitarbeitern festgenommen.

Maaandamano ya wajerumani Mashariki waliokua wakidai uhuru wa kusafiri

Ukuta ulipoporomoka miaka 20 iliyopita,watu wote waliduwaa.Urusi pia.Katibu mkuu Mikhael Gorbatschow alikawia kuarifiwa.Hakuna aliyeweza kuashiria hali ya mambo katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani -GDR-ingechukua sura gani -hata shirika la upelelezi la KGB halikuweza.

Jumatatu ya November tisaa mwaka 1989,balozi wa Urusi katika jamhuri ya kidemokrasi ya Ujerumani-GDR,Wjatscheslaw Kotschemassow alitaka kumpigia simu mkubwa wake,waziri wa mambo ya nchi za nje Edouard Schewardnadse.Hali inatisha:Serikali ya Berlin Mashariki inataka kuwarahisishia shughuli za usafiri wananchi wake waweze kuingia Shirikisho la jamhuri ya Ujerumani na anataka kujua kama Usovieti haina pingamizi.Mjini Moscowa lakini hakuna anaejibu simu:

Sababu kwamba hakuna anaejibu simu pengine inatokana na ile hali kwamba siku chache kabla watu nchini Soviet Union walikua wakisherehekea miaka 72 ya mapinduzi ya October.Viongozi wa serikali hawapatikani.Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje,ambae hakua akijua cha kufanya,akaruhsu,wafanye kile wanachotaka kufanya "marafiki zao" kama wenyewe warusi na wajerumani mashariki walivyokua wakijiita zamani.

Magharibi ilipowadia,watumishi wa ubalozi wa Urusi wakafuatilizia katika televisheni mkutano aliokua nao Günter Schabowski pamoja na waandishi habari.Walishtuka walipomsikia mwanachama huyo wa kamati kuu ya kisiasa akitangaza kufunguliwa ukuta.Kwasababu ruhusa ya Moscow ilihusiana na kuvuka mpaka wa Ujerumani tuu kuingia jamahuri ya Tcheki.

"Nijuavyo mie,ruhusa hiyo inaanza tangu sasa."Amesema Günter Schabowski.

Memoclick Brandenburger Tor beim Mauerfall am 09.11.1989

Katika lango la Brandenburg ukuta ulipoporomoka November 9 mwaka 1989

Hapo ikazuka hali ambayo kwa mtazamo wa leo mtu anaweza kusema si ya kawaida.Badala ya kumuarifu moja kwa moja katibu mkuu wa chama cha kikoministi cha Usovieti-Mikhael Gorbatchov,balozi wa Usovieti aliyeonyesha amechoka, Kotschemassow,akaamua kumeza vidonge vya usingizi-na kulala hapo hapo.Saa chache baadae,maelfu ya wajerumani mashariki walipoanza kuongozana kuingia Berlin Magharibi,msaidizi wake Igor Maximiytschew alijikuta akikabiliwa na kizungumkuti kikubwa:kimsingi alilazimika kuwapigia simu viongozi wa Kremlin na kwa namna hiyo kusababisha jibu la pupa.Maximytschev akawakumbuka wale ambao walipendelea zaidi ufumbuzi wa kichina,yaani jeshi liingilie kati na kutumia nguvu kama ilivyotokea katika uwanja wa Tiananmen, mjini Beijing,miezi michache kabla,ili kulivunja nguvu vuguvugu la waliokua wakidai demokrasia.Ingawa Gorbatschov aliondowa uwezekano kama huo,lakini simu ya kutoka Berlin,tena saa za usiku,ingeangaliwa kama ishara mambo yanatisha.Balozi wa Urusi lakini aliamua vyengine.

Hata watumishi wa idara ya upelelezi ya Urusi waliduwaa.Iwan Kusmin alikua wakati ule, mkuu wa idara ya habari ya KGB.Yeye aliangalia televisheni na kuona mkutano wa Shabowski pamoja na waandishi habari.Lakini alifikiri hauna umuhimu mkubwa,akenda kulala.Aliamshwa saa sita za usiku na maafisa wa makao makuu ya KGB ya Berlin-Karlshorst na kuarifiwa kwamba mipaka imefunguliwa.

Mwandishi:Gonscharenko,Roman/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul-Rahman

 • Tarehe 19.10.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KAFj
 • Tarehe 19.10.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/KAFj
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com