Mgomo wa wauguzi mjini Berlin | Magazetini | DW | 25.09.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Mgomo wa wauguzi mjini Berlin

Huduma za afya sakosolewa sawa na unavyokosolewa mfumo wa sasa wa shughuli za kiuchumi nchini Marekani

default

Mjadala wa bunge kuhusu bajeti ya mwaka 2009

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wamejishughulisha na vuta vikuvute ya kidiplomasia kati ya Marekani na Urusi,mzozo katika masoko ya hisa na kuhusu matatizo katika hospitali za Ujerumani.

Tuanzie Ujerumani ambako gazeti la Die Welt linaandika:

"Maelfu kwa maelfu ya wauguzi ,madaktari wanaharakati wa vya wafanyakazi na wawakilishi wa mashirika kadhaa ya huduma za afya wanateremka majiani hii leo mjini Berlin.Wanalalamika dhidi ya sera za afya ambazo wafanyakazi wa hospitali wanahisi hazivumiliki.Hali ya kuzorota shughuli za utawala katika sehemu chungu nzima,itaendelea kuwepo licha ya serikali kuu kupitisha kitita cha mabilioni ya fedha kusaidia kurahisisha shughuli hizo.Kwasababu miundo mbinu ndiyo iliyooza.Bajeti iliyokubaliwa na bunge tangu miaka 16 iliyopita haikidhi mahitaji ya fedha yanayozidi kuongezeka.Na mageuzi katika sekta ya afya nayo pia yanazidi kukorofisha mambo.Yuro bilioni tatu zilizoahidiwa na waziri Schmidt,mzigo utakaowangukia wenye bima za afya na walipa kodi,hazitakua na faida yoyote si kwa wagonjwa na wala si kwa wauguzi."

"Mzigo utamuangukia mwenye bima ya afya" ndio kichwa cha maneno cha gazeti la FLENSBURGER TAGEBLATT,linaloendelea kuandika:

"Mpango huo unaudhi hasa kwasababu miundombinu haijafanyiwa marekebisho.Ikilinganishwa na kwengine ulimwenguni,basi mtu ataona kwamba nchini Ujerumani huduma katika vituo vya afya na katika hospitali ni za juu mno na zinagharimu fedha nyingi.Mashindano zaidi yanahitajika miongoni mwa hospitali na zahanati ili kuinua bidii na ufanisi."

Gazeti la MÄRKISCHE ZEITUNG la mjini FRANKFURT an der ODER linahoji:

"Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita,wauguzi zaidi ya 50elfu wameachishwa kazi.Na hata kama sambamba na kufutwa nafasi za kazi,idadi ya hospitali imepunguzwa,lakini idadi ya wagonjwa imeongezeka.Kwa namna hiyo idadi ya wagonjwa wanaoshughulikiwa na muuguzi mmoja imeongezeka mara dufu.Na hata ikiwa nafasi 21 elfu zaidi zitabuniwa,hazitatosha kujaza pengo lililoko."

magazetini inahusu mzozo katika masoko ya fedha unaosababisha hivi sasa kuingilia kati idara ya utafiti wa ndani nchini Marekani FBI.Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG linaandika:

"Hakuna ushahidi bado.Lakini kuna ripoti kwamba FBI wanazichunguza taasisi 26 za fedha katika soko la hisa la Wall Street,kama benki zote zimekua zikitoa hesabu za uwongo au kama baadhi tuu ya mameneja ndio waliokua wakiwahadaa wateja wao.Sio Marekani tuu,ulimwengu mzima unachora picha mbaya ya ubepari hivi sasa.Kila kitu kinawezekana.Lakini kinyume na namna ilivyokua katika kashfa nyengine za fedha,wanaowasaka wahalifu watakua na shida ya kupata ushahidi bayana au hata kuwafichua wanaiohusika na kashfa hiyo.Kiini cha mzozo wa sasa ni ukosefu wa sheria zinazoweza kusimamia shughuli za kibiashara katioka soko la hisa la wall Street."

Gazeti la TAGESZEITUNG linazungumzia mpango wa serikali ya Marekani wa kuinusu hali ya kiuchumi nchini humo."Mkubwa kupita kiasi" anasema mhariri wa gazeti hilo na kuendelea kuandika:

"Tatizo sio dala bilioni 700 za walipa kodi zitakazomiminwa katika benki na mashirika ya bima.Sekta hiyo kweli inahitaji msaada wa haraka.Tatizo lakini linakutikana katika masharti ya mpango huo wa uokozi:patazuka muimla wa shughuli za fedha,yaani waziri wa fedha.Pendekezo la sheria linazungumzia juu ya kutoguswa mtu huyo na ukaguzi wowote si wa bunge na wala si wa mahakama.Zaidi ya hayo chanzo cha mzozo hakijashughulikiwa.Ikiwa wanasiasa hawatobuni mbinu mpya za shughuli za kiuchumi,basi msaada wao wa mabilioni utamalizikia kuzinusuru benki kuu.Na kwa namna hiyo zitaendelea na shughuli zao kama zamani na kuwacheka wanasiasa." • Tarehe 25.09.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FOmb
 • Tarehe 25.09.2008
 • Mwandishi Hamidou, Oumilkher
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/FOmb
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com