1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merkel ataka hatua kali zaidi kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi

Halima Nyanza(ZPR)4 Julai 2011

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua thabiti na za lazima duniani kote, kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

https://p.dw.com/p/11oMv
Kansela Angela MerkelPicha: dapd

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira mjini Berlin, hapa Ujerumani, uliowashirikisha wawakilishi kutoka nchi 35, kansela Merkel amesema haitoshi tu, kwa nchi zenye viwanda kupunguza gesi chafu, kwa ajili ya kujaribu kupunguza ujoto duniani.

Petersberger Klimadialog Berlin Klimaschutz
Waziri wa Mazingira wa Ujerumani Norbert Roettgen(Katikati) akifungua mkutano huoPicha: picture alliance / dpa

Amewaambia washiriki wa mkutano huo kwamba bado hakujapatikana makubaliano mengine yatakayoweza kuchukua nafasi ya azimio la Kyoto, ambalo linamaliza muda wake mwaka ujao.

Mkutano huo unaendelea leo, chini ya Uenyekiti wa wenyeji Ujerumani, na Afrika kusini, nchi ambayo mkutano ujao wa mabadiliko ya tabia ya nchi, unatarajiwa kufanyika.