Mataifa ya Ghuba yatakiwa kuibana Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 08.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mataifa ya Ghuba yatakiwa kuibana Iran

MANAMA

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Robert Gates ameyataka mataifa ya Ghuba yaishinikize Iran kubainisha dhamira zake zilizopita za kutaka kutengeneza silaha za nuklea na kuapa hadharani kutotengeneza silaha hizo huo mbeleni.

Gates amewataka viongozi wa mataifa hayo kushirikiana pamoja kuilazimisha Iran kukomesha urutubishaji wa madini ya uranium na kuisaidia serikali dhaifu ya Iraq .

Gates amesema popote unapoangalia unakutana na sera ya Iran ya kuchochea ukosefu wa utulivu na machafuko bila ya kujali kumwagika kwa damu ya watu wasiokuwa na hatia.

Gates alikuwa akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa usalama mjini Manama Bahrain .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com