Ufaransa, Ubelgiji kuitambua Palestina kama taifa
22 Septemba 2025
Kando ya Ufaransa, Ubelgiji na New Zealand zimeshatangaza au kuashiria kuitambua Palestina kama taifa. Jumapili 21.09.2025, Uingereza, Canada na Australia zilikuwa miongoni mwa mataifa ya magharibi kuitambua Palestina.
Awali, akitangaza mpango wa kuitambua Palestina kama taifa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema, "Tutatangaza kuitambua Palestina kama nchi, suala ambalo ni mwanzo wa mchakato wa kisiasa na mpango wa amani na usalama kwa kila mtu."
Ujerumani kwa upande wake kupitia Waziri wake wa mambo ya nje Johann Wadephul, imesema juhudi za kupata suluhisho la mataifa mawili ya Israel na Palestina zinapaswa kuanza mara moja. Wadephul anatazamiwa pia kushiriki katika mkutano wa mataifa mengine ya magharibi yanayopanga kuutambua utaifa wa Palestina.