Marekani imewatambua waasi Libya | Matukio ya Kisiasa | DW | 16.07.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Marekani imewatambua waasi Libya

Marekani imejiunga na mataifa mengine makuu yenye nguvu duniani katika kulitambua baraza la kitaifa la waasi nchini Libya kuwa taasisi halali ya uongozi nchini humo.

default

Mkutano wa kundi la mashauriano kuhusu Libya, mjini Istanbul Uturuki

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton alitangaza hayo katika mkutano mjini Istanbul Uturuki, wa zaidi ya mataifa 30 na taasisi za kimataifa, zijulikanazo kama kundi la mashauriano kuhusu Libya. Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza William Hague amesema kundi hilo liliahidi kuwaunga mkono waasi hao katika jitihada zao za kutaka kumuondoa uongozini Muammer Gaddafi.

Hillary Clinton Washington Pressekonferenz

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary clinton

Kutambuliwa baraza hilo la waasi huenda kukasababisha kutolewa fedha nyingi. Uturuki imesema dola bilioni 3 za mali ya Libya zilizozuiliwa zitatolewa , ili muradi fedha hizo zitumike kwa sababu za kibinadamu pekee. Makubaliano ya baraza la usalama la Umoja wa mataifa pamoja na vikwazo vya kimataifa dhidi ya utawala wa Gaddafi, vimezuia fedha za Libya katika nchi za nje. Gaddafi anakataa kujiuzulu na amesema atapigana hadi mwisho.

Mwandishi: Maryam Abdalla,AFP, dpa, Reuters
Mhariri: Kitojo,Sekione

DW inapendekeza

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com