1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni:Tetemeko kujiuzulu Kramp-Karrenbauer halikutisa tu CDU

Sekione Kitojo
11 Februari 2020

Mzozo  unaokikumba  kwa  hivi  sasa  chama  tawala  cha  CDU ni mzozo  uliopo ndani ya  siasa  za  Ujerumani. Na  kuanzia sasa madaraka ya  Angela  Merkel katika  chama  hicho  yamepotea.

https://p.dw.com/p/3XaGH
Berlin CDU Pressekonferenz Annegret Kramp-Karrenbauer
Picha: Getty Images/AFP/O. Andersen

Kujiuzulu kwa  mwenyekiti wa  chama cha  CDU Annegret Kramp-Karrenbauer  na  kujitoa  kwake  kuwa mgombea wa  kiti cha kansela wa  Ujerumani, ni kutokana  na  kutojiamini, katika  chama ambacho  kimeanza  kukosa  mwelekeo. Lakini  tetemeko  hilo linafika  mbali.

Chama  cha  CDU kimejikwaa. chama  kingine  kikuu  cha  SPD, kwa muda  mrefu  sasa  kinatafuta  mwelekeo, kinatafuta  kisimamie wapi, kinatafuta msingi  wake.  Kama  ilivyokuwa  kwa  kiongozi  wa chama  cha  SPD  Andrea Nahles mapema  katikati  ya  mwaka 2019  baada  ya  miezi 13  tangu  kuingia  katika  uongozi  wa chama  hicho  kikongwe  nchini  Ujerumani , sasa  Kramp-Karrenbauer  nae  ametangaza  kujiuzulu baada  ya  miezi 14  tu madarakani.

Nini  kinachofuata  baada  ya  hapa ? Majina, majina , majina, uvumi na  matarajio. Lakini  swali kuhusu  nani  atakiongoza  chama  hicho hapo  baadaye  na  nani  anaweza  kuwa  mgombea  wa  wadhifa wa  kansela linaendelea  kuwapo. Chama  kinapaswa  kuweka  wazi kuhusu kujitambua  pamoja  na  umoja  wao.

Kwasababu kwa  muda  mrefu  sasa  CDU  inaonekana  kuwa  si chama  kilichokuwa  pamoja , katika  jimbo  la  Thuringia na Ujerumani kwa  jumla , katika  mitandao na kazi  zake  za  kila  siku, kwa  kuwa  kila mara   kinaonekana  kuwa  na  mivutano.

Wiki kumi  na  moja  zimepita, baada  ya  mkutano  wa  kila  mwaka wa  chama  cha  CDU mjini  Leipzig  na  kilimshangilia  Kramp-Karrenbauer kuwa  kiongozi  wake, na  baada  ya  ukosoaji  mkubwa dhidi  yake.

Deutsche Welle Strack Christoph Portrait
Mwandishi wa uhariri huu Christoph StrackPicha: DW/B. Geilert

Ujerumani  katika  mwaka  mmoja  ujao inakabiliwa  na  uchaguzi mkuu.

Utakuwa uchaguzi  utakaoamua sio tu kuhusu  suala, la iwapo  lakini pia  ni vipi chama  cha  CDU  na  vyama  vinavyounda  serikali vitabakia  katika  uongozi ama  vinaweza kubakia. Suala  litakuwa kuhusu  wabunge, umuhimu  wa  vyama, nidhamu  ya  chama pamoja na  uhuru wa  wabunge. Na  mjadala ni kuhusu swali, iwapo  na  vipi vyama  vya  siasa za  wastani  vinaweza kupata  nguvu  na kupambana  na  vyama  vile vinavyolemea  siasa  za  kizalendo.

Sababu  alizotoa  Kramp-Karrenbauer kuhusiana  na  uamuzi wake uliokuja  na  kimbunga  kikali  kwa jamii, ni kwamba  CDU  yenye nguvu  inahitaji uongozi  imara. Hatimaye hali  inahusu  hali  ya baadaye  ya  demokrasia  nchini  Ujerumani.

Karibu miaka  71 baada  ya  kuundwa  jamhuri  ya  watu  wa Ujerumani  inaingia  katika  majaribu  makubwa, pengine inawezekana  ni mwanzo  wa  mwisho  wa  mfumo  wake  wa vyama. Suala  lingine, ni kuhusu  chama  imara  cha  walinzi  wa mazingira, cha  kijani, kama  kitaweza  ama  la  kuchukua  jukumu la vyama  vya  hivi  sasa  vikuu  vya  umma.