1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Annegret Kramp-Karrenbauer

Annegret Kramp-Karrenbauer, wakati mwingine akiitwa kwa ufupisho wa majina yake kama AKK, ni mwanasiasa wa Ujerumani na waziri wa sasa wa ulinzi tangu Julai 2019 na mwenyekiti wa chama cha CDU tangu 2018.

AKK alikuwa Katibu Mkuu wa chama cha Christian Democratic Union CDU, waziri mkuu wa jimbo la Saarland kuanzia 2011-2018, akiwa mwanamke wa kwanza kuongoza serikali ya Saarland, na mwanamke wa nne kuongoza serikali ya jimbo la Ujerumani. Kramp-Karrenbauer anachukuliwa kuwa mhafidhina aneegemea zaidi upande wa kijamii, lakini yuko upande wa kushoto wa CDU kuhusu sera ya kiuchumi. Ndie mwanamke wa pili kushika wadhifa wa waziri wa ulinzi nchini Ujerumani.

Onesha makala zaidi