Maoni ya wahariri juu ya ″silaha kwa waasi wa Syria″ | Magazetini | DW | 28.05.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya "silaha kwa waasi wa Syria"

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya kimsingi wamekuabliana kundoa vikwazo vya silaha dhidi ya Syria.Maana ya hatua hiyo ni kwamba nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kuwapelekea silaha wapinzani wa serikali.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle wakati wa mkutano juu ya Syria

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle,wakati wa mkutano juu ya Syria

Mhariri wa gazeti la "Landeszeitung" ana mashaka juu ya uamuzi huo.Unauliza jee ni sawa silaha kuingia katika mikono ya watu wenye itikadi kali? Na jee itawafiki na maadili ya Ulaya kumwangusha Assad ambae utawala wake unatenganisha dini na siasa? Mhariri huyo anasema zimwi likujualo halikuli likakwisha! Anasema juu ya Syria,Umoja wa Ulaya unahitaji jawabu la makini.

Mhariri wa gazeti la "Nürnberger"anaiunga mkono hoja hiyo kwa kusema kwamba katika muktadha wa kushtadi kwa mgogoro baina ya Wasuni na Washia nchini Sryia,haitakuwa hatua ya busara kupeleka silaha kwa waasi kama Uingereza na Ufaransa zinavyodhamiria. Mhariri wa "Nürnberger"anasema siyo jambo la busara kupeleka silaha kwa watu usiowajua,ambao wanaweza kuziekeleza kule kusikojulikana!

Mkutano baina ya waasi na serikali ya Syria:

Gazeti la"Offenburger Tageblatt" linazungumzia juu ya mkutano unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao ili kuujadili mustakabal wa Syria. Wajumbe wa Assad na waasi wanatazamiwa kushiriki kwenye mkutano huo.Juu ya mkutano huo gazeti la "Offenburger Tageblatt"linatoa maoni yake kwa kueleza washiriki kwenye mkutano huo watapaswa kufikia mwafaka juu ya kuijenga Syria mpya bila ya Assad na genge lake.

Hadi wakati wa kufanyika mkutano huo, Umoja wa Ulaya utapaswa uachane na wazo la kupeleka silaha Syria ili kuepusha mgogoro kufikia hatua ya kutoweza kudhibitika na pili kuepuka kuzuia njia bora ya kuutatua mgogoro wa Syria yaani ya kupeleka ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani.Mauaji na madhila yanayowasibu watu nchini Syria lazima yakomeshwe.

Ujerumani na China:

Mhariri wa gazeti la "Badische"anatoa maoni yake juu ya uhusiano baina ya Ujerumani na China baada ya Waziri Mkuu wa China Li Keqiang kufanya ziara nchini Ujerumani. Mhariri wa gazeti hilo anatahadharisha juu ya ushirika baina ya nchi mbili hizo. Anasema ushirika wa istihaki baina ya watu wawili siku zote una kanuni zake.Faida ya upande mmoja inakuwa hasara ya upande mwingine. Hivyo ndivyo ilivyo katika ushirika wa pande mbili.

Yapasa kutambua kwamba Waziri Mkuu wa China anatafuta mshirika barani Ulaya ili kuzuia ushuru wa adhabu wa mabapa ya nishati ya jua, ya bei rahisi yanayouzwa barani Ulaya kutoka China. Na kwa hivyo itakuwa vizuri ikiwa serikali ya Ujerumani itatambua kwamba China inatupa chambo!

Mwandishi:Mtullya Abdu./ Deutsche Zeitungen.

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman