MANAMA: Iran ipo tayari kuisaidia Marekani kuondosha vikosi Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 09.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MANAMA: Iran ipo tayari kuisaidia Marekani kuondosha vikosi Irak

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Manouchehr Mottaki amesema,Iran ipo tayari kuisaidia Marekani kuhamisha vikosi vyake kutoka Irak,ikiwa Washington itabadilisha msimamo wake kuhusu Iran. Alipozungumza nchini Bahrain,waziri Mottaki alisema,vikosi vya kigeni vilivyoikalia Irak vinabeba lawama ya takriban nusu ya machafuko yanayotokea nchini humo.Kwa maoni ya Mottaki,eneo zima litanufaika kama Marekani itaviondosha vikosi vyake kutoka Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com