1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

magazetini hii leo nchini Ujerumani

19 Agosti 2004

Mkutano pamoja na waandishi habari uliofanywa na kansela Gerhard Schröder baada ya kumalizika kipindi cha mapumziko ya msimu wa kiangazi ndio mada iliyohanikiza ndani ya magazeti ya Ujerumani hii leo.Hata kuingia katika soko la hisa kampuni la Google ni miongoni mwa yale yaliyodhukuriwa magazetini hii leo.

https://p.dw.com/p/CHPj

Uchambuzi wa nusu njia ,ikimaanisha miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2006,ndio uliofanywa na kansela wakati wa mkutano pamoja na waandishi habari,akiitumia fursa hiyo kutetea kwa mara nyengine tena mageuzi ya soko la ajira.Gazeti la Frankfurter ALLGEMEINE Zeitung limemvulia kofia lilipoandika:

"Yeyote yule aliyeamini,kansela wa shirikisho angerejea tena jukwaani mjini Berlin akiwa amepwaya baada ya wiki kadhaa za mapumziko na mastarehe nchi za nje,ameula na chua."Mkutano huo uliogeuka kua jambo la kawaida,ambapo kansela Gerhard Schröder huzungumza na waandishi habari baada ya serikali kurejea toka likizoni,umetoa picha ya kiongozi aliyepania kweli kweli: kiongozi mkakamavu,mwenye matumaini na asiyekua na taharuki,picha inayopingana moja kwa moja na hoja pengine angejitokeza kama kiongozi aliyedhoofika na kuduwaa kutokana na maandamano ya majiani .

Gazeti linalosomwa na wengi la mjini Cologne,Express lina maoni sawa na hayo.Limeandika:

"" Hajawahi kuonekana vile tangu muda mrefu uliopita.Kansela Schröder amejitokeza kua mcheshi,amepumuwa na mwenye kupenda mzaha."Hakuna ishara ya mtu aliyekatishwa tamaa kutokana na kichaa na kitisho cha baragumu dhidi ya mageuzi katika soko la ajira mashuhuri kwa jina Hertz nambari nne.Kinyume chake ndicho kilichoshuhudiwa:Schröder amebainisha wazi wasi,hajali kura za maoni ya umma zinazoachiria kuporomoka umashuhuri wa serikali yake na chama chake cha SPD,ataendelea na siasa yake na kutekeleza mageuzi kama ilivyopangwa.:

Gazeti la Abendzeitung la mjini München linajiuliza:

"Kama hali ya kujiamini na kujiwekea matumaini iliyojitokeza,kansela Schröder aliporejea mjini Berlin,itasaidia kweli kuleta ufanisi,ni jambo la kusubiri na kuona hasa tukizingatia jinsi jamii inavyohangaika.Hata hivyo, jinsi alivyopania,watu wasimchezee ,anaweza kuitanabahisha jamii na kujikingia pointi zaidi pamoja na chama chake,seuze tena ameshasema "mageuzi hayo hayana badala."

Gazeti la Lüneburger LANDESZEITUNG linahisi

"Ikiwa hadi wakati huu,kansela alikua akichekelea lilipohusika asuala la mageuzi katika sekta ya jamii,hivi sasa mambo yamebadilika anaonyesha amepania kweli kweli kuyatekeleza.Ukakamavu huu unampa nguvu zaidi kuwashinda wapinzani wake wa CDU na CDU,wanaojaribu kupitia maandamano ya kila jumatatu,kuficha ukweli kwamba na wao pia wanabeba jukumu la mpango huo wa mageuzi.Zaidi ya hayo,msimo wa kansela Schröder wa kuendeleza liwe liwalo mageuzi ni dalili njema kwa mila za kisiasa humu nchini.

Gazeti la Frankfurter Rundschau lina maoni kinyume na hayo,linahisi

"Schröder hakuelewa kabisa kipi kinawasumbuwa wananchi.Hana hila kuweza kuwatanabahisha wananchi.Hana,baada ya maneno matamu,lolote linaloweza kutuliza hofu zilizozagaa miongoni mwa jamii katika eneo la mashariki ya Ujerumani.Hana antenna ya kupunguza ghaadhabu zilizosababishwa na Hartz nambari nne.Ameahidi tuu mageuzi yatachambuliwa kwa kina na kwamba hakauna njia ila kuyatekeleza.Anakiangalia kua ni ahadi kile ambacho wengi wanahisi ni kitisho.

Na hatimae gazeti la mjini Düsseldorf la kibiashara Handelsblatt limemulika pirika pirika za kuingia katika soko la hisachombo cha utafiti katika mtandao wa internet Google.Gazeti limeandika

"Kutokana na milolongo ya misuko suko iliyogubika kuingia Google katika soko la hisa,wengi katika soko kuu la hisa la wall Street wanazungumzia hivi sasa juu ya balaa.Hukmu hiyo inastahiki hasa mtu akizingatia patashika iliyofuatana na uamuzi wa Google kuingia katika masoko ya hisa.