1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Virusi vya maradhi ya midomo na miguu kwa wanyama huenda vilisambazwa na binaadamu

8 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBb8

Virusi vilivyosababisha vilivyosabisha mlipuko wa maradhi ya midomo na miguu katika mashamba mawili ya mifugo huko kusini mwa Uingereza huenda vilitoka katika maabara iliyojirani na maeneo hayo.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa kamati ya usalama wa afya ya Uingereza.

Imesema kuwa huenda vilisambazwa na binaadamu, na kusema kuwa uwezekano wa hewa kuchangia kusambaza virusi hivyo ni mdogo.

Virusi hivyo vilibainika kwa mara ya kwanza Ijumaa wiki iliyopita, kabla ya taarifa ya kubainika katika shamba la pili la mifugo juzi jumatatu.

Mashamba yote mawili ya mfugo yako kilomita chache kutoka katika maabara ya serikali pamoja na ile inayoendeshwa na kampuni binafsi ya madawa.