1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kura ya maoni yaonesha CDU/CSU zafungana na AfD

31 Januari 2026

Muungano wa vyama vya kihafidhina wa Kansela wa Ujerumani, Friedrich Merz, uko sawa na chama cha mrengo mkali wa kulia, Alternative for Germany (AfD), kwa mara ya kwanza katika miezi kadhaa, kwa mujibu wa utafiti INSA.

https://p.dw.com/p/57o0e
Ujerumani Berlin 2026 | Kansela Friedrich Merz katika kikao cha Bundestag
Ujerumani Berlin 2026 | Kansela Friedrich Merz katika kikao cha BundestagPicha: dts Nachrichtenagentur/IMAGO

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa kwa niaba ya gazeti la Bild na kuchapishwa leo Jumamosi, iwapo uchaguzi wa shirikisho ungefanyika kesho, asilimia 26 ya waliohojiwa walisema wangeipigia kura Christian Democratic Union (CDU) ya Merz au chama chake ndugu cha Bavaria, Christian Social Union (CSU). Chama cha AfD pia kimekuwa katika kiwango cha asilimia 26 kwa wiki kadhaa, hali iliyokifanya kuwa mbele ya vyama vinavyounda serikali ya muungano. Mara ya mwisho kwa CDU/CSU kuwa sawa na AfD katika utafiti wa INSA ilikuwa mwezi Septemba 2025. Utafiti wa INSA ulifanywa kati ya Januari 26 na 30, ukihusisha watu 1,204 wenye sifa za kupiga kura nchini Ujerumani, na na kiwango chake cha juu cha makosa kitakwimu kikikadiriwa takriban asilimia 2.9.