Kupanda kwa kiwango cha Joto - Mabadiliko ya hali ya hewa | Noa Bongo | DW | 26.02.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Noa Bongo

Kupanda kwa kiwango cha Joto - Mabadiliko ya hali ya hewa

Viwango vya joto vinazidi kuongezeka barani Afrika, na hivyo kusababisha hali ya ukame, mafuriko na uhaba wa chakula. Sikiliza kwa makini ufahamu jukumu na mchango wako katika kubadilisha hali hii!

Mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha kiwango cha joto kuongezeka

Mabadiliko ya hali ya hewa yanasababisha kiwango cha joto kuongezeka

Ingawa si kosa lako, hali hii inaendelea kutuathiri kwa kiwango kikubwa. Bara la Afrika ndilo litakalo athirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa, licha ya kwamba bara la Ulaya na Marekani ndiyo yanayochangia pakubwa ongezeko la kiwango cha gesi ya Kaboni na moshi angani – chanzo kikubwa cha ongezeko la kiwango cha joto duniani.

Ni bara la Afrika ambalo limo hatarini zaidi kwa sababu, bara hili hutegemea sana kilimo. Sehemu nyingi za bara hili zinakumbwa na ukame, mawimbi ya joto kali na misimu isiyoweza kutabirika, hivyo kuifanya vigumu kuendesha shughuli za kilimo cha aina yoyote.

Je ni vipi unaweza kushirikiana na wengine ulimenguni katika kampeni ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kijijini mwako. Hilo ndilo swali wanalojiuliza Joshua, Carol, Lorna na Alex katika mchezo wa redio Noa Bongo jenga maisha yako kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Ni vijana wannne walioamua kuchukua hatua ya kupinga mradi wa ujenzi wa kiwanda cha umeme kijijini mwao, na mwishowe kujifunza mengi tu ya kushangaza kuhusiana na suala zima la mabadiliko ya hali ya hewa.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘Noa bongo Jenga Maisha yako; vinasikika katika lugha sita: Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Hausa, Kireno na Amharic. Na vinafadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Vilivyopakuliwa