Konare ataka mzozo wa Kenya atafutiwe ufumbuzi | Habari za Ulimwengu | DW | 28.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Konare ataka mzozo wa Kenya atafutiwe ufumbuzi

Katibu mkuu wa Umoja wa Afrika, Alpha Oumar Konare, ametoa mwito mzozo wa kisiasa nchini Kenya utafutiwe ufumbuzi.

Kiongozi huyo ameelezea wasiwasi wake kuhusu machafuko yanayoendelea nchini humo yaliyosababishwa na matokeo ya uchaguzi wa tarehe 27 mwezi Disemba mwaka jana.

Akizungumzia ujumbe wa aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu, bwana Konare amewataka viongozi wajiulize kuhusu jukumu la Rwanda katika mauaji ya halaiki ya mwaka wa 1994 ambapo wanyarwanda takriban laki nane waliuwawa.

Konare alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Umoja wa Afrika wanaokutana mjini Addis Abba nchini Ethiopia kabla kuanza kwa mkutano wa kilele wa nmoja huo Alhamisi ijayo mjini humo.

Huku akiutaka umoja wa Afrika uisaidie Kenya, Konare amesema suluhisho si kugawana madaraka bali kuiheshimu misingi ya utawala bora na kukabiliana na machafuko.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com