Kombe la Afrika Mashariki na kati | Michezo | DW | 14.07.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kombe la Afrika Mashariki na kati

kinyan'ganyiro cha kombe la afrika mashariki na kati chaendelea Dar-es-salaam:Simba yalazwa na Tusker 3-2

Bundesliga-Ligi ya ujerumani ikijiandaa kuanza msimu mpya mwezi ujao, Jürgen klinsmann ashika rasmi usukani wa mabingwa Bayern Munich kama kocha wake mpya.

Kinyan'ganyiro cha kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika ya mashariki na kati kinaendelea leo kwa timu zinazocheza Morogoro,kuingia nazo uwanjani.

Msichana wa kenya mwenye umri wa miaka 18 Jelimo ameshinda mbio zake za 3 za Golden League mjini Athens akimtimua nje mkenya mwenzake Jeneth Jepkosgei-bingwa wa dunia.

Na katika ringi ya mabondia, Wladmir klichko amelitetea taji lake la wezani wa juu ulimwenguni la shirika la IBF.

Hayo na mengineo,ndio niliowaandalia jioni hii:

►◄

Kinyan'ganyiro cha kombe la klabu bingwa kanda ya Afrika mashariki na kati kinaendelea tena leo mjini Dar-es-salaam na Morogoro,Tanzania:

FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni,limethibitisha kwamba mashabiki wa Afrika kusini wataruhusiwa kwenda viwanjani na mazumari yao ya VUVUZELA wakati wa kombe lijalo la dunia 2010. ruhusa ya kuwaachia mashabiki hao kuingia viwanjani na mazumari hayo yenye kelele ilitolewa baada ya mjadala wa masaa kadhaa .

Wakati wa mjadala huo, waandazi wa kombe la dunia nchini walifaulu kuihakikishia FIFA kuwa mazumari hayo ni sehehu ya desturi halisi za dimba humo nchini.

FIFA awali ikihofia kwamba, mazumari hayo yaweza kutumiwa kama silaha na wahuni au wanabiashara kutembeza bidhaa zao viwanjani.

Stadi wa kiungo wa timu ya taifa ya Uholanzi anaeichezea Hamburg katika Bundesliga, Rafael van der Vaart, amekanusha mwishoni mwa wiki ripoti kwamba Real Madrid ya Spian yataka kumuajiri.

"yamkini wana hamu na mimi, lakini hakuna mazungumzo tuliofanya." -Alisema van der vaart aliporejea kwa mazowezi na klabu yake ya Hamburg kujiandaa kwa msimu mpya.

Gazeti la kila siku la michezo la Spain -Marca liliripoti alhamisi iliopita kwamba Real Madrid imetoa kitita cha dala milioni 31.6 kumnunua van der vaart.Klabu yake ya Hamburg pia imkanusha kupokea taarifa zozote kutoka Real.

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ugiriki, NikosLiberopolous

amefunga mkataba wa miaka 2 na klabu ya bundesliga Eintracht Frankfurt.

Mshambulizi huyu mwenye umri wa miaka 32 anajiunga na Frankfurt kwa mkataba wa hadi 2010 kutoka klabu ya ugiriki ya AEK Athens.

Mabingwa wa Ujerumani Bayern munich tangu Julai mosi, wana kocha mpya-nae ni Jürgen klinsmann,mchezaji wao wa zamani na aliekua kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani katika kombe lililopita la dunia ,aliiongoza Bayern munich mwishoni mwa wiki katika mechi yake ya kwanza na klabu ya daraja 3 kama sehemu ya mazowezi ya msimu mpya.

Klinsmann alisema:

"Hii ni klabu yenye mila na utamaduni uliodumu karne nzima.Ni klabu iliotoa mastadi na viongozi mashuhuri.Nina fahari kua nami sasa nimepata fursa kutoa mchango wangu."

Munich inalenga tena katika msimu mpya wa Bundesliga unaoanza mwezi ujao kutwaa vikombe vitatu-viwili nyumbani na kombe la Ulaya la champions League.

Klabu ya Liverpool ya Uingereza, imemuajiri kipa wa Brazil Diego Cavalieri anaeichezea klabu ya Palmeiras.Kipa huyo mwenye umri wa miaka 25,amefunga mkataba wa miaka 4 na Liverpool.

RIADHA:

Michezo ijayo ya Olimpik ikikaribia mwezi ujao, wanariadha kote ulimwenguni wamekuwa wakijinoa katika mashindano ya Grand Prix:

Mjini Athens, Ugiriki wanariadha wa masafa mafupi wa jamaica wameendelea kutamba: Usain Bolt, bingwa wa rekodi ya dunia ya masafa ya mita 100, alikimbia jana mjini Athens, muda wa kasi kabisa mwaka huu katika masafa ya mita 200.

Chipukizi huyu mwenye umri wa miaka 21 alivunja rekodi ya dunia ya mjamaica mwenzake Asafa Powel hapo kabla na jana alikimbia muda wa dakika 19.67 kwa masafa ya mita 200.

Muafrika kusini Louis Van Zyl ameshinda mbio za mita 400 kuruka viunzi wakati mkenya Ezekiel Kemboi , alishinda mbio za mita 3000 kuruka viunzi.Tareq Mubarak wa Bahrein alitokea wapili wakati Hamid Ezzine wa Morocco akiridhika na nafasi ya tatu.

Upande wa wasichana, Eunice Jepkorir wa Kenya alinyakua ushindi huku Zemzem Ahmed wa Ethiopia akafuata nafasi ya pili na Ruth Bisibori Nyangau pia wa Kenya akitokea 3.

MABONDIA:Muukraine aliepiga maskani yake Ujerumani, Wladmir Klitschko ametetea mwishoni mwa wiki mjini hamburg, taji lake la wezani wa juu ulimwenguni la shirika la IBF na WBO baada ya kumdengua katika duru ya 11 muamerika Tony Thompson.Klitschko alifufuka kutoka duru za kwanza za msukosuko na kummaliza hasimu yake katika duru ya 11 kwa konde kali la kulia.