1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kinyanyang'anyoro cha mkurugenzi mpya wa WTO chaendelea

18 Septemba 2020

Kinyanyang'anyoro cha kumtafuta mkurugenzi mkuu mpya wa Shirika la Biashara Duniani, WTO kinaendelea kushika kasi huko Geneva, Uswisi.

https://p.dw.com/p/3ifvb

Leo hii shirika hilo litayatangaza majina matatu ambayo yatakwenda katika duru ya kupigiwa kura, baada ya kuwafyeka wagombea kutoka Mexico, Misri na Moldova. Mchujo wa leo unawahusu wagombea kutoka mataifa ya Uingereza, Korea Kusini, Nigeria, Kenya na Saudi Arabia. Upi mtazamo wa wachambuzi kuhusu mchakato huo? Hilo ni swali ambalo Sudi Mnette amemuuliza mchumi Dokta Bravious Kyahoza akiwa Dar es Salaam, Tanzania.