1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kifungo cha miaka 20 kwa Meja wa zamani wa Rwanda

P.Martin6 Julai 2007

Mahakama nchini Ubeligiji imetoa kifungo cha miaka 20 kwa Bernard Ntuyahaga aliekuwa afisa wa jeshi la Rwanda.

https://p.dw.com/p/CHBW

Adhabu hiyo imetolewa kwa mauaji ya wanajeshi 10 wa Kibeligiji yaliyotokea mwaka 1994.Wanajeshi hao wa Kibeligiji walikuwa sehemu ya vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa na waliuawa siku moja baada ya ndege ya rais wa Rwanda kuangushwa tarehe 6 mwezi wa Aprili mwaka 1994.Kufuatia mauaji ya wanajeshi hao wa Kibeligiji,Umoja wa Mataifa uliondoa vikosi vyake kutoka Rwanda.Katika mauaji yaliyofuata,kiasi ya watu 800,000 waliuawa na Wahutu wenye siasa kali. Wengi waliouawa,walikuwa wa kabila la wachache la Watutsi na pia Wahutu wa siasa za wastani.