KHARTOUM:Vikosi vya serikali vyavamia kambi ya Kalma | Habari za Ulimwengu | DW | 22.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM:Vikosi vya serikali vyavamia kambi ya Kalma

Uvamizi wa vikosi vya serikali ya Sudan katika kambi ya Kalma umezusha hali ya wasiwasi katika eneo la magharibi kabla ya kufanyika mazungumzo ya amani.

Makundi ya waasi yanailaumu serikali ya Sudan kwa kutumia nguvu kuwahamisha takriban wakaazi milioni mbili wanaoishi katika kambi za eneo hilo.

Watu 19 kutoka kambi hiyo ya Kalma wametiwa nguvuni na polisi kwa tuhuma za kuhusika na mashambulio dhidi ya vituo vya polisi kusini mwa jimbo la Darfur.

Mkuu wa polisi wa kusini mwa Darfur Omar Mohamed Ali amesema kwamba watu hao wanashukiwa kushiriki katika shambulio la jumapili lililo muuwa askari mmoja na kuwajeruhi askari wanane.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com