KHARTOUM: China na Sudan zatia saini mikataba ya biashara | Habari za Ulimwengu | DW | 03.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: China na Sudan zatia saini mikataba ya biashara

Rais Hu Jintao wa China na rais Omar el Bashir wa Sudan wametia saini mikataba kadhaa ya biashara. Mikataba hiyo inahusika na sekta za mawasiliano, nishati na miundo mbinu.Baadae vile vile rais Hu alisema anaunga mkono mpango wa kupelekwa vikosi vya pamoja vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika jimbo la Darfur,kama njia ya kumaliza mapambano katika eneo hilo la mgogoro, magharibi mwa Sudan.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa,si chini ya watu 200,000 wameuawa na milioni 2 wengine wamelazimika kuondoka makwao tangu mapigano kuzuka katika jimbo la Darfur, miaka minne ya nyuma.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com