Kesi ya ICC kuhamishwa Kenya? | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Kesi ya ICC kuhamishwa Kenya?

Kundi la watawala nchini Kenya wanataka kuona kesi dhidi ya watu mashuhuri wanaoshukiwa kuhusika na machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, zikitoweka.

ARCHIV - Das Gebäude des Internationalen Strafgerichtshofs (IStGH) in Den Haag (Archivfoto vom 29.03.2004). Der IStGH will am Mittwoch (04.03.2009) bekanntgeben, ob er gegen den sudanesischen Präsidenten Al-Baschir Haftbefehl wegen des Verdachts auf Kriegsverbrechen und Völkermord in der sudanesischen Krisenprovinz Darfur erlässt. Foto: Toussaint Kluiters (zu dpa 0282 vom 03.03.2009) +++(c) dpa - Bildfunk+++

Makao makuu ya ICC mjini The Hague

Kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, mjini The Hague, Uholanzi, huenda zikaathiri makundi makuu mawili ya kikabila, katika kinyang'anyiro cha kudhibiti urais. Tangu Kenya ilipopata uhuru wake mwaka 1963, nchi hiyo kimsingi inatawaliwa na familia tatu tajiri kutoka makabila ya Kikuyu na Kalenjin. Miongoni mwa watu sita wanaokabiliwa na uwezekano wa kufikishwa mahakamani The Hague, wawili ni kizazi kipya cha viongozi kutoka makundi hayo mawili na wote wawili wameshasema kuwa watagombea uchaguzi wa rais mwakani.

Makundi yanayotawala nchini Kenya, yanamuunga mkono waziri wa fedha, Uhuru Kenyatta ambaye ni Mkikuyu na mtoto wa muasisi wa Kenya Jomo Kenyatta. Hata William Ruto wa kabila la Kalenjin aliezuiliwa kwa muda, kama waziri wa elimu ya juu, ili aweze kushughulikia kesi yake inayohusika na rushwa anaungwa mkono na watu hao. Wote wawili wanashukiwa na ICC kuhusika na machafuko yaliyozuka kufautia uchaguzi wa Desemba 2007. Watu 1,300 waliuawa na maelfu wengine walipoteza makaazi yao wakati wa machafuko hayo.

Opposition leader Raila Odinga, left, looks on as Kenyan President Mwai Kibaki, right, announce the cabinet and Odinga as the Prime Minister, Sunday, April 13, 2008 at State House in Nairobi, Kenya. President Mwai Kibaki on Sunday named rival Raila Odinga as prime minister, implementing a power-sharing deal after protracted negotiations over the deal they signed over a month ago.(AP Photo/Karel Prinsloo)

Rais Mwai Kibaki(kulia) na Waziri Mkuu Raila Odinga wa Kenya

Ikiwa washukiwa hao wawili watashtakiwa rasmi mjini The Hague, basi hiyo huenda ikampatia mwanasiasa mashuhuri asiekuwemo katika makundi ya watawala, fursa ya kudhibiti urais. Huyo ni Waziri Mkuu Raila Odinga. Yeye ni Mluo na familia yake na kabila lake wamekuwa kama ni maudhi kwa viongozi wa Kenya tangu nchi hiyo kujipatia uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1963.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa Odinga anashika nafasi ya mbele katika kinyangányiro cha kumrithi Rais Mwai Kibaki, anaepaswa kuondoka kisheria. Katika uchaguzi wa mwaka 2007, Odinga alidai kunyanganywa ushindi na Kibaki na machafuko yakaibuka. Wawekezaji na wafadhili wanaifuatiliza mada hiyo kupima kiwango cha mageuzi ya kisiasa yatakayostahmiliwa na viongozi wa Kenya na kujua nani alie na nafasi ya kushinda uchaguzi wa rais katika nchi yenye uchumi mkubwa kabisa katika Afrika ya Mashariki.

Kibaki alie Mkikuyu alimrithi Daniel Arap Moi wa kabila la Kalenjin. Na yeye alipokea wadhifa wa rais kutoka kwa Jomo Kenyatta. Kwa wapiga kura wengi nchini humo, utiifu wa kikabila ni muhimu kuliko mitazamo ya kisiasa. Rais Kibaki akikaribia kuondoka, makundi ya kikabila yanayotawala yanajiandaa kwa kila njia. Marais wa nchi kadhaa za Kiafrika wanaombwa kuisaidia Kenya kuishawishi The Hague kuzifungua kesi hizo mjini Nairobi. Lakini makundi ya haki za binadamu yana wasiwasi kuwa lengo halisi la serikali ni kuwaachilia huru washukiwa hao ikiwa kesi hizo hatimae zitahamishwa Nairobi. Lakini serikali inakanusha kabisa tuhuma hiyo.

Mwandishi: P.Martin/RTRE
Mpitiaji: Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com