Kesi dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya mwanahabari yakosolewa | Habari za Ulimwengu | DW | 23.05.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kesi dhidi ya watuhumiwa wa mauaji ya mwanahabari yakosolewa

-

KINSHASA

Hukumu ya kifo dhidi ya watu watatu walioshtakiwa kwa mauaji ya mwandihsi habari wa kituo cha redio Okapi cha Umoja wa Mataifa nchini Jahmhuri ya kidemoksri ya Kongo imekosolewa vikali na mashirika ya haki za binadamu .Kamishna anayehusika na masuala ya haki za binadamu katika Umoja wa mataifa Louise Arbour amekosoa jinsi kesi hiyo ilivyoendeshwa akisema mahakama ya kijeshi imeshindwa kutafuta kweli juu ya mauji hayo.Aidha amekosoa hali ya kutumiwa mahakama hizo ambazo zinaendelea kuwahukumu raia katika ukiukaji wa sheria za kimataifa na katiba ya Kongo.Mwanahabari Serge Maheshe mwenye umri wa miaka 31 aliuwawa kwa kupigwa risasi mjini Bukavu mwezi Juni mwaka jana.

Waandishib wa habari wasiojali mipaka pamoja na mashirika mengine ya habari nchini Kongo pia yamekosoa kesi hiyo.Kamati ya kimataifa ya kuwalinda waandishi wa habri iliyo na makao yake mjini New York Marekani imezungumzia wasiwasi wake juu ya suala hilo ikisema kwamba lengo la kuuwawa kwa mwandihsi habari huyo bado halijajulikana.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com