Kenya: Kujiuzulu kwa Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Moses Wetangula | Matukio ya Kisiasa | DW | 27.10.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Kenya: Kujiuzulu kwa Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Moses Wetangula

Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya, Moses Wetangula, amesema kwamba anajiuzulu huku kukiweko madai ya ufisadi dhidi yake katika ishara za hivi karibuni za kupambana na jambo hilo.

Bunge la Kenya ambako mahojiano yaliendelea kuhusu mkasa wa waziri wa mambo ya kigeni Bw.Wetangula

Bunge la Kenya ambako mahojiano yaliendelea kuhusu mkasa wa waziri wa mambo ya kigeni Bw.Wetangula

Bwana Wetangula alisema amefanya uamuzi wa kibinafsi wa kujiweka kando kama waziri wa mambo ya kigeni ili kutoa nafasi kwa wale wanaomuandama, na pia kutoa nafasi kwa uchunguzi ufanyike kutokana na tuhuma hizo. Alihakikisha kwamba atarejea katika baraza la mawaziri punde pale uchunguzi utkapokamilika, kwa vile anajua yeye hana makosa.

Punde hivi Othman Miraji alimuuliza kwa njia ya simu waziri mwenzake, Profesa Anyang' Nyong'o, wa huduma za afya, kuhusu hatua ya Moses Wetangula...

Mwandishi: Othman Miraji

Mpitiaji: Josephat Charo

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com