Jumuiya ya Afrika Masharika yakua
18 Juni 2007Matangazo
Marais hao wanatarajiwa kuzindua rasmu wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vilevile kumuapisha Julias Tangus Rotich makamu mpya wa Katibu Mkuu. Aidha rais Yoweri Museveni wa Uganda anapokea rasmu uwenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Rais Mwai Kibaki wa Kenya.
Rwanda na Burundi zilijiunga na Jumuiya hiyo mwezi Novemba mwaka jana na kusubiri uanachama kamili kuanza mwezi Julai.