1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Assange akubaliwa kupinga hukumu ya kuhamishwa Marekani

Amina Mjahid
20 Mei 2024

Muasisi wa tovuti ya Wikileaks Julian Assange ameshinda ufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama moja ya Uingereza iliyoidhinisha apelekwe Marekani kusikiliza kesi yake dhidi ya Uvunjifu wa sheria ya usalama wa kitaifa.

https://p.dw.com/p/4g4rN
Uingereza | Mwasisi wa WikiLeaks Julian Assange |
Mwasisi wa WikiLeaks Julian Assange.Picha: Maja Smiejkowska/REUTERS

Muasisi wa tovuti ya kuvujisha nyaraka za siri Wikileaks Julian Assange ameshinda nafasi ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama moja ya Uingereza iliyoidhinisha apelekwe Marekani kusikiliza kesi yake dhidi ya Uvunjifu wa sheria ya usalama wa kitaifa.

Majaji wawili wa mahaka ya juu mjini London walimpa Assange nafasi ya kukata rufaa  baada ya awali kuitaka Marekani ithibitishe kutoa hakikisho la kulinda  uhuru wa kujieleza katika kesi yoyote inayohusu taifa  hilo.

Soma pia: Biden asema anatafakari ombi la Australia la kuifuta kesi dhidi ya muasisi wa Wikileaks Assange

Assange aliye na miaka 52 hakuwepo mahakamani wakati uamuzi huo ulipotolewa.

Jullian Assange anatuhumiwa kuchapisha nyaraka nyingi za siri za Marekani. Kwa miaka mingi, Australia imekuwa ikiitolea wito Marekani kuitupilia mbali kesi yake dhidi ya Assange, raia wa Australia ambaye anapinga juhudi za Marekani kutaka ahamishiwe nchini humo kutoka gereza la Uingereza.