1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Jibu la Urusi kwa mali yake iliyofungiwa na Marekani

23 Mei 2024

Urusi itatambua mali ya Marekani pamoja na dhamana, ambazo zinaweza kutumika kama fidia kwa hasara iliyopatikana kutokana na kufungiwa kwa mali yake nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/4gDIw
Waandamanaji wakiwa na mabango katikati mwa jiji la London kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Waandamanaji wakiwa na mabango katikati mwa jiji la London kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.Picha: TOLGA AKMEN/AFP/Getty Images

Urusi itatambua mali ya Marekani pamoja na dhamana, ambazo zinaweza kutumika kama fidia kwa hasara iliyopatikana kutokana na kufungiwa kwa mali yake nchini Marekani. Haya ni kulingana na amri iliyotiwa saini leo na Rais wa nchi hiyo Vladimir Putin.

Amri hiyo inaidhinisha tume ya serikali ya Urusi kuhusu mauzo ya mali za kigeni kutambua mali na majimbo husika ambayo maamuzi ya fidia yatafanyiwa mahakamani.

Amri hiyo ya leo iliorodhesha dhamana, mali isiyohamishika na mali zinazohamishika pamoja na hati miliki miongoni mwa mali zinazomilikiwa na Marekani zinazoweza kufungiwa.

Soma pia:  Zelensky: Ukraine inapata mafanikio ingawa hali bado ngumu uwanja wa vita

Mali ya wawekezaji wengi wa kigeni, ikiwa ni pamoja na watu binafsi na hazina kuu za uwekezaji za Marekani, zinazuiwa katika akaunti maalumu  'type-C' ambazo Urusi ilianzisha muda mfupi baada ya kutuma vikosi vyake nchini Ukraine na kuwekewa mfululizo wa vikwazo vya Magahribi mnamo Februari mwaka 2022.

Pesa katika akaunti hiyo haziwezi kuhamishwa nje ya Urusi bila idhini kutoka kwa mamlaka ya Urusi.