1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Zelensky: Ukraine inapiga hatua lakini hali bado ni ngumu

Sylvia Mwehozi
22 Mei 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wanajeshi wake wanapata mafanikio yanayoridhisha dhidi ya vikosi vya Urusi katika eneo la kaskazini mashariki mwa mkoa wa Kharkiv.

https://p.dw.com/p/4g7rw
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian Presidency/abaca/picture alliance

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema wanajeshi wake wanapata mafanikio yanayoridhisha dhidi ya vikosi vya Urusi katika eneo la kaskazini mashariki mwa mkoa wa Kharkiv. Kupitia hotuba yake ya kila siku, Zelensky hata hivyo ameonya kuwa pamoja na mafanikio hayo, hali bado ni ngumu sana upande wa mashariki mwa eneo la mapambano karibu na miji ya Pokrovsk, Kramatorsk na Kurakhove.Zelensky anatarajia Urusi itaimarisha mashambulizi yake upande wa kaskazini

Hayo yanajiri wakati Urusi ikianza luteka za kijeshi za silaha za nyuklia karibu na Ukraine, katika kile ilichosema ni jibu dhidi ya "vitisho" vya nchi za Magharibi, baada ya Kyiv kutoa wito kwa washirika wake kudungua makombora ya Urusi kutoka kwenye maeneo yao.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock aliyewasili mjini Kyiv jana, alisema kuchelewesha misaada kwa Ukraine kunatoa kitisho cha usalama kwa nchi za magharibi.