ISLAMABAD:Musharraf apingana na mjumbe wa Marekani juu ya hali ya hatari
18 Novemba 2007Matangazo
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Negroponte amemtaka rais Musharraf aondoe hali ya hatari aliyotangaza nchini Pakistan mapema mwezi huu.
Lakini jenerali Musharraf amejibu kwa kusema kwamba hali ya hatari itondolewa ikiwa usalama utaimarika nchini mwake.
Mjumbe huyo wa Marekani aliwasili nchini Pakistan siku moja baada ya kuzungumza kwa njia ya simu na kiongozi wa upinzani Benazir Bhutto alieachiwa huru ijumaa iliyopita baada ya kuzuiwa nyumbani katika mji wa Lahore.