Iran yakanusha madai ya Marekani kuhusu kisa cha manuari zake na mataboti za Iran | Habari za Ulimwengu | DW | 09.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Iran yakanusha madai ya Marekani kuhusu kisa cha manuari zake na mataboti za Iran

TEHRAN:

Jeshi la kimapinduzi la Iran limeilaumu Marekani kwa kubuni picha za video kuonyesha kuwa mataboti za Iran zikisumbua manuari za kijeshi za Marekani katika mlango wa bahari wa Hormuz.

Jumanne,jeshi la Marekani lilitoa mkanda wa Video ukionyesha mataboti za Iran zikikaribia manuari za Marekani na kuzitishia kuzilipua.Jeshi la kimapinduzi la Iran linasema, mkanda huo umebuniwa tu.Kituo cha televisheni cha kiarabu cha Iran-Al-Alam pia kimetoa tangazo la kukana likinukuu duru za jeshi la kimapinduzi.Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitoa video ya dakika nne ikionyesha kile maafisa wa Marekani walichokiita mvutano uliodumu dakika 20.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com