HANOI:Mvua za Monsoon zasababisha mafuriko | Habari za Ulimwengu | DW | 09.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HANOI:Mvua za Monsoon zasababisha mafuriko

Maafisa nchini Vietnam wamesema idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko katika eneo la Kati nchini humo imeongezeka na kufikia zaidi ya watu 40 ambapo kiasi cha watu 13 hawajulikani waliko.

Mafuriko hayo yalisababishwa na mkua kubwa zilizonyesha katika eneo hilo la pwani ya Vietnam mapema wiki hii.

Wakati huo huo maafisa katika eneo la kusini mwa Asia wamesema zaidi ya watu 2000 huko India Bangladesh na Nepal wameuwawa kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua za muda mrefu kuanzia mwezi juni.

Waziri wa mambo ya ndani amesema kiasi cha vijiji 6500 vinakabiliwa na mafuriko katika jimbo la Bihar lakini hali inaendelea kuimarika.Maeneo mengine yaliyoharibiwa na mafuriko hayo ni Uttar Pradesh na Assam.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com