Hali ya umasikini unaozidi Ujerumani . | Magazetini | DW | 19.05.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Hali ya umasikini unaozidi Ujerumani .

Vipi kupiga vita umasikini ni shina la maoni ya wahariri leo:

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani, leo yametuwama mno juu ya mada za ndani na hasa juu ya tarakimu zilizochapishwa kuhusu hali ya umasikini nchini upande wa wakaazi wanyonge:Maoni hayo ya wahariri yamegusia pia juu ya mtetezi wa chama cha SPD kwa uchaguzi ujao wa rais bibi Gesine Schwan na kukanusha kuwa utawala wa kidikteta wa iliokua Ujerumani Mashariki (GDR), haukuwa dola lisilofuata sheria.

Gazeti la Stuttgarter Nachrichten kuhusu tarakimu zilitzoka juu ya umasikini unaongezeka Ujerumani, laandika:

"Kupata mapato ya chini wananchi hakutakoma kwa njia ya kila kukicha serikali inagawanya fedha zaidi, bali kwa kuhakikisha kazi zinakuwapo na mpya zinapatikana.Hii inazidi kuwa taabu katika mkoa wa kusini-magharibi.Iwapo chama cha wafanyikazi kinataka kupiga vita umasikini huko,basi hakifai kuutoa maanani mpango wa kuustawisha uchumi."

Tarakimu za hali ya umasikini zilizotolewa zinatia dosari sherehe za kuadhimisha miaka 60 tangu kuundwa kwa Shirikisho la jamhuri ya ujerumani zilizopangwa jumamosi hii.Kugawanya kisiasa kwa Ujerumani kulimalizika miaka 20 iliopita,mwanya kati ya masikini na matajiri unazidi ,kupanuka. Sio tu Ujerumani mashariki a na magharibi bado zimegawika ,bali hata sehemu ya kusini ya Ujerumani ilioneemeka inaendelea kujitenga na kaskazini ilio maskini na mikoa mipya ya mashariki."

Ama gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG linahisi umasikini humu nchini kinyume na ule katika nchi changa ambako kwa wakaazi wake wengi una maana kujipatia alao mlo kuweza kuishi ,katika nchi tajiri kama Ujerumani si jambo nadra bali ni la kawaida.gazeti laongeza:

"Kwa watawala yafaa sasa kuzindukana kengele ya hali ya hatari imelia.....Kile kitakachosaidia kweli kukomesha hali ya umasikini, ni kutoa nafasi za kazi katika maeneo yalioathriwa mno na ufukara."

Gazeti la NEUE OSNABRUCKER ZEITUNG likitukamilishia mada hii laonya:

"Hasa katika nyakati hizi za kinyanganyiro cha kuania hali bora, jumuiya zinazowahudumia wanyonge zapaswa kuongeza nguvu zao hasa kwa wale hali zao za kiuchumi ni duni. Bado tufauti za maeneo na za kijamii ni kubwa.Kwa jicho la hali ulimwenguni na hata la ulaya, si hali ya kutisha.Ili hali isalie hivyo, panahitajika sera ya kuwahudumia wanyonge ambayo itatambua kuwa hakuna nchi inayomudu mfumo wa kutoa huduma kwa wonyege ambako kwa kila mkaazi wake ni ghali mno,lakini haukidhi kusawazisha tofauti katika jamii kama huu wa Ujerumani ulivyo."

Gazeti la Norwest Zeitung kutoka Oldenburg linayachambua matamshi ya mtetezi wa wadhifa wa urais wa Ujerumani wa chama cha SPD Bibi Gesine Schwan.Laandika:

"Ikiwa mtetezi huyo wa chama cha SPD anapinga kuiita iliokua Ujerumani Mashariki ni ni nchi ya kidikteta ambayo "haikuheshimu sheria" ,

bali hafichi kuwa anajitembeza ili kupata kura za chama cha mremngo wa shoto cha LINKSPARTEI pale kura zitakapopigwa Bungeni.Si ajabu basi, kuona wapinzani wa zamani na pia washirika wenzake chamani kutoka mashariki waliojionea binafsi dhulma ,wameijitokeza kumpinga bibi Schwan.

Muhimu zaidi kuliko hasira hizo ziliozooneshwa kwa matamshi hayo, ni kwa uongozi wa chama cha SPD kutoa tangazo rasmi.La sihivyo, shaka shaka zitazidi kuwa matamshi hayo, ni mkakati wa kukifungulia chama hiocho mlango zaidi wa kukijongelea chama cha Linke cha mrengo wa shoto kwa jicho la uchaguzi ujao."

Mtayarishaji:Ramadhan Ali/ DPA

Mhariri:M.Abdul-Rahaman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com