Hali ya uandikishaji kwa wapiga kura visiwani Zanzibar
14 Septemba 2009Matangazo
Zoezi la kuandikisha wapiga kura kwenye daftari la kudumu la wapiga kura Visiwani Zanzibar limeahirishwa kwa leo, huku wananchi wakiwa na wasiwasi kutokana na hali ya usalama kisiwani Pemba. Hata hivyo kabla ya kufungwa kwa vituo vya kujiandikisha, wananchi walitawanywa kwa mabomu ya kutoa machozi na maji ya kemikali.
Grace Kabogo alizungumza na mwandishi wetu Salma Said akiwa kisiwani Pemba na alianza kwa kusema hali halisi ya usalama ilivyo kwa sasa kisiwani humo.