Gordon Brown asema hatohudhuria mkutano wa Afrika na Ulaya | Habari za Ulimwengu | DW | 27.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gordon Brown asema hatohudhuria mkutano wa Afrika na Ulaya

LONDON.Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kuwa hatoudhuria mkutano wa kilele kati ya wakuu wa afrika na Ulaya utakaofanyika tarehe 8 na 9 mwezi ujayo huko Ureno.

Brown amesema hayo baada ya Rais Robert Mugabe kunukuliwa akisema kuwa atahudhuria mkutano huo Lisbon.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema kuwa haiwezekani kwao kuhudhuria mkutano huo na kukaa pamoja na Mugabe.

Rais Mugabe anatuhumiwa na nchi za magharibi zikiongozwa na Uingereza kwa kile zinachosema uvunjaji wa haki za binaadamu na demokrasia.

Umoja wa Ulaya umemuwekea vikwazo vya kusafiri kiongozi huyo wa Zimbabwe.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com