Gaza.Kijana wa miaka 17 auwawa na mashambulio ya Israel huko Gaza. | Habari za Ulimwengu | DW | 06.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza.Kijana wa miaka 17 auwawa na mashambulio ya Israel huko Gaza.

Kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 17 na mwanamgambo mmoja wameuwawa huko Gaza hii leo wakati Israel iliposhambulia maeneo ya Wapalestina.

Mashambulizi hayo ya Israel yaliyoanza siku sita zilizopita, yamepelekea kuuwawa kwa Wapalestina 52 na mwanajeshi mmoja wa Israel kuuwawa.

Aidha Mashambulizi ya Israel katika mamlaka ya Wapalestina ambayo yalianzia miezi minne iliyopita na kupelekea zaidi ya Wapalestina 300 kuuwawa baada ya mwanajeshi wao kutekwa njara, yanalaumiwa na jumuiya za kimataifa.

Mwanafunzi Mahmud Ashafi ameuuliwa na Wapalestina wengine tisa, wawili kati yao wakiwa na umri wa miaka mitano wamejeruhiwa wakati ndege za kijeshi za Israel ziliposhambulia katika mji wa Beit Lahiya, kaskazini mwa Gaza.

Mashahidi wamesema, wanamgambo ambao ndio waliokuwa wamelengwa walikimbia lakini makombora ya Israel yalipopiga karibu na basi lililokuwa limebeba wanafunzi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com