GAZA:Hamas waanza harakati za kumkomboa mwandishi | Habari za Ulimwengu | DW | 03.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Hamas waanza harakati za kumkomboa mwandishi

Wanamgambo wa kundi la Hamas wamelizingira eneo ambapo anashikiliwa mwandishi wa habari wa Uingereza Alan Johnston kwa miezi minne sasa.

Kiasi cha wapiganaji elfu sita wa Hamas wameyazingiza majengo katika eneo la Gaza ambapo mwandishi huyo anashikiliwa na kundi la jeshi la kiislam linaloongozwa na koo ya Doghmush.

Msemaji wa Wizara ya Ndani, Khaled Abu Hilal amesema kuwa majeshi ya usalama hayatabakiza kitu katika msako huo mpaka mwandishi huyo anapatikana.

Kituo cha Radio cha Hamas pia kimetangaza namba ya simu ambayo mtu akipiga hachajiwi kuweza kutoa habari zitakazosaidia kupatikana kwa mwandishi huyo.

Kundi hilo dogo la jeshi la kiislam ambalo zamani lilikuwa na uhusiano na kundi la Hamas, linadai Uingereza kumwachia mwanaharakati wa siasa kali za kiislam na kutishia kumuua mwandishi huyo iwapo Hamas watajaribu kutumia nguvu kumuokoa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com