GAZA CITY: Makundi hasimu ya Kipalestina yapambana karibu na Chuo Kikuu | Habari za Ulimwengu | DW | 27.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY: Makundi hasimu ya Kipalestina yapambana karibu na Chuo Kikuu

Makundi hasimu ya Kipalestina yamepambana kwenye Ukanda wa Gaza karibu na Chuo Kikuu cha Kiislamu kinachounga mkono chama cha Hamas.Si chini ya watu 2 waliuawa katika mapambano hayo.Vile vile katika mfululizo wa utekaji nyara mpya,wanachama 4 wa kikosi cha usalama kinachomuunga mkono Rais Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah,walitekwa nyara na watu wenye silaha wasiojulikana.Sasa idadi ya watu waliofariki kutokana na mapigano ya siku ya Ijumaa imefikia 17.Kwa sababu ya mapambano hayo mapya,majadiliano kati ya Fatah na Hamas yenye azma ya kuunda serikali mpya ya Wapalestina yenye umoja wa kitaifa yameahirishwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com