DUSHANBE.waandamanji wameapa kuendelea na shinikizo za kumtaka rais wa nchi hiyo ajiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 03.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUSHANBE.waandamanji wameapa kuendelea na shinikizo za kumtaka rais wa nchi hiyo ajiuzulu

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank- Walter Steinmier amewasili nchini Tajikstan akiwa ziarani katika nchi za Asia ya kati.

Waziri Steinmier anatarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo Rahmonov katika mji mkuu wa Dushanbe.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmier baadae ataelekea nchini Kirygystan ambako maelfu ya waandamanaji wameapa kuendelea na maandamano katika mji wa Bishkek leo hii kumlazimisha rais Kurmanbek Bakiyev ajiuzulu.

Maandamano hayo yalianza tangu jana wakati rais Bakiyev aliposhindwa kuwasilisha mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo yenye kifungu kinacho mpunguzia uwezo katika mamlaka yake ya urais.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com