DUBAI:Zawahiri atishia mashambulio zaidi dhidi ya Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 11.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DUBAI:Zawahiri atishia mashambulio zaidi dhidi ya Uingereza

Kiongozi nambari mbili katika mtandao wa kigaidi wa Alqaeda Ayman Al Zawahiri ametishia mashambulio zaidi dhidi Uingereza kufuatia hatua ya nchi hiyo kumtunuku cheo cha heshima mwandishi vitabu Salman Rushdie.

Katika ukanda wa sauti uliotumwa kwenye tovuti ya mtandao huo Zawahiri ameishutumu Uingereza kwa kuwa wanafiki kwa kumpa heshima ya utu bora mwandishi huyo kwa jina la uhuru wa kutoa maoni.

Zawahiri amemshutumu malikia Elizabeth akisema ametoa ujumbe wazi kwa waislamu kwa kumvika heshima mtu aliyeutukana uisilamu katika kitabu chake cha beti za shetani.

Kitabu hicho kiliwakasirisha mno waislamu baada ya kuchapishwa mara ya kwanza mwaka 1988 na kusababisha kutaka kumuua jambo ambalo lilimlazimu Rushdie kuishi mafichoni kwa muda wa miaka tisa.

Matamshi ya Zawahiri yamekuja siku kadhaa baada ya mashambulio yaliyoshindwa kwenye miji ya London na Glasgow.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com