DRESDEN : Chama cha Merkel chatafuta umoja wa chama | Habari za Ulimwengu | DW | 27.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

DRESDEN : Chama cha Merkel chatafuta umoja wa chama

Chama cha kihafidhina cha Kansela Angela Merkel kinataka kuwasilisha msimamo wa pamoja wakati wanachama wake wakikutana leo hii katika mji wa Dresden katika mkutano ambao utachagua tena uongozi wa chama hicho.

Chama cha Christian Demokrat CDU cha Merkel kimeiongoza Ujerumani kwa mwaka mmoja uliopita katika serikali ya mseto ya muungano mkuu na chama cha Social Demokrat cha Kansela aliemtangulia Gerhard Schroeder.Uchunguzi wa maoni katika miezi ya hivi karibuni umeonyesha umashuhuri wa chama hicho umekwama uko chini ya asilimia 35 inayokatisha tamaa ambayo ilikuwa nayo wakati iliposhinda uchaguzi hapo mwaka jana.

Matokeo hayo yamekuja baada ya mazungumzo ya mageuzi makubwa ya kiuchumi kuwaudhi wananchi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com