DHAKA: Ghasia zazuka kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa zamani, Bangladesh
29 Desemba 2006Matangazo
Watu kadhaa wamejeruhiwa kaskazini mwa Bangladesh baada ya polisi kukabiliana na wafuasi wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Hossain Mohammad Ershad.
Majeshi yalipelekwa kuzima ghasia zilizotokea wakati wa maandamano katika mji wa Rangpur anakotokea Mohammad Ershad na wilaya za jirani.
Ghasia hizo zilisababishwa na hatua ya serikali kumkataza rais huyo wa zamani kibali cha kugombea uchaguzi wa mwezi ujao.
Polisi walitumia gesi za kutoa machozi pamoja na risasi za mpira kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe na vijiti.
Siku ya jumanne, Mahakama kuu iliamua kuendelea kwa kifungo cha miaka miwili cha Ershad kwa hatia ya ufisadi.