1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dakar. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani analiza ziara yake huko Senegal na kwenda Sudan.

21 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEsQ

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice ametumia ziara yake ya kwanza katika bara la Afrika akiwa kama waziri jana kuonesha nia mkubwa iliyonayo Marekani kwa makubaliano ya biashara na bara hilo masikini zaidi duniani.

Katika ziara ambayo ilipangwa kulenga juhudi za kuepusha ghasia zaidi katika mashariki ya kati na jimbo la Dafur nchini Sudan , Rice amesema kuwa mpango wa Marekani wa ukuaji wa kiuchumi wa bara la Afrika na fursa unaojulikana kama AGOA umewafaidisha watu wengi.

Rice amewaambia waandishi wa habari kuwa mpango huo umeweza kubadilisha maisha ya watu wengi pamoja na misaada ya maendeleo, utawala bora na uwekezaji mitaji moja kwa moja kutoka mataifa ya kigeni.

Mara baada ya mkutano huo na waandishi wa habari Bibi Rice aliondoka na kuendelea na ziara yake nchini Sudan.