1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAsia

China yalaani meli za Marekani, Uingereza kupita Taiwan

13 Septemba 2025

China imeilaani kitendo cha Marekani na Uingereza kutumia eneo tete la Mlango Bahari wa Taiwan kupitisha meli zao za kivita muda mfupi baada ya kutangaza kuwa meli yake ya tatu ya kijeshi, imepita pia kwenye sehemu hiyo.

https://p.dw.com/p/50QRE
Mgogoro wa China na Taiwan
Meli ya jeshi la wanamaji ya Marekani USS Halsey katika Mlango Bahari wa TaiwanPicha: Ismael Martinez/U.S. Navy/AP)/picture alliance

Msemaji wa kamandi ya mashariki wa jeshi la China Kanali Shi Yi amesema vikosi vya anga na vya wanamaji vya China vilifuatilia mwenendo wa meli mbili za Marekani na Uingereza na kudai zilidhoofisha amani na utulivu eneo hilo.

Marekani na Uingereza zinautazama Mlango Bahari wa Taiwan kama eneo la maji ya kimataifa linaloweza kutumiwa na meli kutoka mataifa yote. Hata hivyo China inadai Taiwan ni sehemu ya himaya yake na inadai mamlaka katika eneo la maji linalotenganisha Kisiwa hicho kinachojitawala na China bara.